Jumamosi, 25 Novemba 2017

RAIS MAGUFULI: NARUDIA TENA,JENGO LA TANESCO LAZIMA LIBOMOLEWE

 

Rais wa jamhuri ya Muunganao wa Tanzania ,John Pombe magufuli amesisitiza kwamba jengo la shirika la umeme Tanzania (TANESCO) lililopo Ubungo ambalo lipo katika hifadhi ya barabara lazima libomolewe.

Rais magufuli ametoa msisitizo huo leo wakati akizindua hospitali ya taaluma ya tiba Mloganzila mkoani pwani.

Pia amesema kwamba wakati akiwa waziri wa ujenzi alipanga kulibomoa jengo hilo lakini waziri mkuu wa kipingi kile,Mizengo Pinda alimkataza.
 
"Najua wakati ule mizengo pinda kwenye hili alinipinga lakini leo hawezi kunipinga kwa sababu mimi ndiye Rais,".JPM

"Lile jendo la TANESCO narudia ambalo lipo ndani ya road reserve , kama ni kubomoka nusu  au lote lazima ".JPM


Hakuna maoni: