Jumapili, 26 Novemba 2017

PAPA AIZURU MYANMAR INAYOTUHUMIWA KWA MAUAJI YA WAISLAMU WA ROHINGYA


Papa Francis anaanza ziara ya wiki nzima nchini Myanmar na Bangladesh leo Jumatatu, wakati wasiwasi unaendelea wa kimataifa kuhusu usalama na ulinzi kwa wasilamu wa Rohingya.

Anatarajiwa kukutana na Aung Sun Suu Kyi na mkuu wa jeshi Myanmar.

Hata kabla ya kuondoka Roma, Papa Francis alikuwa anakabailiwana kitendawili cha kidiplomasia: iwapo kuliita kundi dogo la waislamu Myanmar - Rohingya.

Ni jina lisilo tumika na serikali ya kiraia na jeshi - wakieleza kuwa ni wahamiaji haramu kutoka Bangladesh na kwahivyo hawapaswi kuorodheshwa kama mojawapo ya makabila nchinihumo.

Lakini mashirika ya kutetea haki za binaadamu wanamuomba awaite hivyo, yakieleza kuwa nilazima Papa Francis aoneshe huruma kwa watu walionyimwa uraia na tangu Agosti wamekabiliwa na kile kamishna wa haki za binaadamu katika Umoja wa mataifa amekitaja kuwa 'kinachoonekana kuwa mauaji ya kikabila'.

Amnesty:Burma yatega mabomu kuwazuia RohingyaMapungufu ya UN katika mzozo wa RohingyaWapiganaji wa Rohingya watangaza kusitisha mapigano, MyanmarMyanmar yatakiwa kukoma kuwatesa Waislamu wa Rohingya

Zaidi ya WaRohingya 600,000 wamekimbilia mpakani - na wakimbizi wakielezea kukabiliwa na mauaji, ubakaji na kuteketezwa moto kwa vijiji - jeshi imekana tuhuma zote.

Papa atakutana na kiongozi wa Myanmarr - Aung Sun Suu Kyi - Jumanne - huenda ni jukumu zito kidiplomasia katika miaka yake minne kama kiongozi wa kanisa katoliki.



Hakuna maoni: