Alhamisi, 2 Novemba 2017

Mwakibinga amvaa Nyalandu

James Mwakibinga Kada wa Chama cha Mapinduzi na mjumbe wa UVCCM
Kada wa Chama cha Mapinduzi na mjumbe wa UVCCM James Mwakibinga afunguka na kumshauri aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Mh. Lazaro Nyalandu Kuacha siasa na kujikita katika mashindano ya ulimbwende.

Mwakibinga Amesema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa wanasiasa waliopoteza dira na muelekeo katika serikali ya awamu ya tano hawana nafasi katika chama.

“Sababu alizotoa kuwa CCM imepoteza dira ni uongo mtupu unapaswa kupuuzwa na katika serikali hii ya awamu ya tano hauna nafasi” alisema

Hata hivyo kumekuwa na maneno yanayosemwa na baadhi ya viongozi waliopo CCM kupitia mitandao ya kijamii hayana budi kupuuzwa na huku wanaendelea kushughulikiwa najua watakimbilia huko.

Niwashauri wanasiasa mchezo umebadilika hivyo wanatakiwa kuwa makini na kuchapa kazi ndiyo njia pekee itakayo waacha salama sio maneno na vijembe wanavyotoa pindi wakosapo nyadhifa fulani katika serikali, alisisitiza Mwakibinga.

Hakuna maoni: