Na Cheji Bakari,Korogwe
MRADI mkubwa wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 913 wa kuleta maji katika mji mdogo wa Mombo Korogwe vijijini unatarajiwa kutekelezwa wiki hii na mkandarasi kampuni ya Pivotech Co.Ltd
Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Korogwe Dk. George Nyaronga amesema kuwa mradi huo mpaka kukamilika utanufaisha wakazi 25,000 katika vijiji vya mji mdogo wa Mombo.
Mradi huo utaanzia katika chanzo cha maji cha kata ya Vuga wilayani Lushoto kwenye milima ya Usambara kupitia Mombo na Mombo Mlembule.
Mradi huo ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2012 na kutarajiwa kukamilika mwaka 2014 ulisimama kwa muda kutokana na kutokea mgogoro katika moja ya vijiji ambavyo ndiyo chanzo cha maji kilitakiwa kuwepo.
" Mradi huu ulianza mwaka 2012 na kutarajiwa kukamilika mwaka 2014 lakini ulikuja kusimama baada ya kutokea mgogoro katika kijiji kimoja katika kata ya Vuga ambapo walikataa kuwepo chanzo" alisema mkurugenzi huyo.
Aidha amesema baada ya makubaliano na wanavijiji wa Vuga tayari wizara ya maji kupitia kwa mkurugenzi wa maji vijijini ameleta mchoro mpya katika utekelezaji wa mradi huo.
Awali mkandarasi huyo katika mwaka 2012 alishalipwa fedha shilingi milioni 320 kwa cheti ambapo awali alilipwa milioni 240 na awamu nyingine akalipwa shilingi milioni 80.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni