Ijumaa, 17 Novemba 2017

Moto mkubwa waathiri kwa kiasi kikubwa jengo la bunge la Cameroon

Moto mkubwa uliotokea katika jengo la bunge la Cameroon umeathiri kwa kiasi kikubwa jengo hilo mjini Yaounde.

Moto huo umeripotiwa kutokea katika usiku wa Alkhamis kuamkia Ijumaa.

Ghorofa nne za juu za jengo la bunge ambapo kunapatikana ofisi za uongozi wa bunge zimeteketea kwa moto huo.

Hakuna mtu yeyote aliefariki katika moto licha ya uharibifu mkubwa uliosababishwa na moto huo.

Siku mbili kabla ya moto huo,  msemaji wa bunge Cavaye Yeguie alisema kuwa ushirikiano baina ya Cameroon na China umepelekea kupatikana kwa jengo jipya la bunge.

Hakuna maoni: