Jumapili, 26 Novemba 2017

Mawakala nane wa Chadema wakamatwa Maswa

Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mh. John Heche amesema jumla ya mawakala 8 wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamekamatwa kwenye uchaguzi mdogo wa kata ya Nyabubinza wilayani Maswa.

“Mawakala wetu kwenye vituo nane kati ya 13 katika kata ya Nyabubinza wamekamatwa na jeshi la polisi na kumekuwa na vitendo vingi tu vya kuharibu uchaguzi”, amesema Heche.

Heche amemtaja Diwani Zakayo Chacha Wangwe kuwa ni miongoni mwa mawakala waliokamatwa wakati zoezi la uchaguzi likiendelea katika hatua ya upigaji Kura.

Aidha John Heche ameongeza kuwa hivi sasa katika vituo hivyo nane ambavyo CHADEMA haina wawakilishi wamebaki mawakala wa vyama vya NCCR na CCM pekee.

Sheria ya Tume ya uchaguzi inakitaka chama kuwasilisha majina ya mawakala siku mbili kabla ya uchaguzi. Chama hutumia nafasi hiyo kuwaandaa mawakala pamoja na kuwaapisha kwajili ya kulinda maslahi ya chama ndani ya uchaguzi. Kwa maana hiyo basi kura katika vituo hivyo zitahesabiwa bila CHADEMA kuwa na wakala.

Hakuna maoni: