Jumamosi, 18 Novemba 2017

Mama huyu avunja rekodi “Madrid Derby” iliyodumu kwa miaka 86

Ukiachana ns ile Derby ya kaskazini mwa London itakayopigwa pale nchini Uingereza hii leo, kule katika ligi kuu nchini Hispania katika dimba la Wanda Metrpolitana kutakuwa na derby nyingine.

Real Madrid ambao msimu huu wanaonekana kuchechemea watakuwa wageni wa Atletico Madrid ambao nao toka msimu uanze wanaonekana kutokuwa vizuri kama ilivyo kwa majirani zao.

Py Laurance anaweza kuwa mtu pekee ambaye anakwenda katika mchezo huu akiwa na presha kubwa kwani hatapenda timu yoyote kati ya Atletico Madrid au Real Madrid ipoteze mchezo wa hii leo.

Py ni mama mzazi wa mlinzi wa kushoto wa Atletico Madrid Theo Hernandez lakini vile vile Py huyuhuyu ndio mama mzazi wa mlinzi wa Real Madrid Lucas Hernandez jambo linalomfanya kushabikia timu zote mbili.

Katika mahojiano na jarida la Marca mwanamama huyu ameeleza kwamba kabla ya mechi ya leo aliwaita na kuwaambia kwamba anawapenda sana na akiwasisitiza wasipigane kwa kuwa wao ni ndugu.

Py anakuwa mzazi wa kwanza kukutanisha watoto wake katika mchezo wa Madrid Derby tangu jambo kama hili lilipotokea katika msimu wa mwaka 1929/1930 na tangu kipindi hicho hakuna aliyeweza kuvunja rekodi hiyo.

Real Madrid na Atletico Madrid wote wana alama sawa (23) na atakayeshinda katika mchezo wa leo atakaa juu ya mwenzake na kupunguza pengo la alama na vinara Barcelona.

Hakuna maoni: