Jumanne, 14 Novemba 2017

Kapombe ateswa na kauli ya Hans Poppe

Uongozi wa klabu ya Simba umeamua kukutana na beki Shomari Kapombe kulimaliza suala la kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe.

Hans Poppe alisema anahitaji kuona Kapombe acheze mpira kwa kuwa amekuwa majeruhi kwa muda mrefu huku akiamini mchezaji huyo amepona.

Kauli hiyo ya Hans Poppe ilizua mjadala mkubwa sana  huku mashabiki wakionyesha kukasirishwa.

Taarifa kutoka ndani ya Simba, zimeeleza, Kapombe atakutana na kaimu Rais wa Simba au kaimu Makamu wa Simba, Iddi Kajuna kulimaliza suala hilo.

Hakuna maoni: