Matatizo ya Everton chini ya Meneja David Unsworth yameendelea kudhihirika baada ya leo tena kuambualia kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Southampton katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la St Marys.
Mshambuliaji wa Saints, Charlie Austin amefunga magoli mawili kwa kichwa katika nusu ya pili ya mechi hiyo, baada ya Dusan Tadic kuwapa wenyeji Southampton uongozi wa mapema.
Mchezaji wa Everton aliyelipiwa gharama ya juu kuliko mchezaji mwingine katika klabu hiyo Gylfi Sigurdsson alisawazisha mambo kabla ya kipenga cha mapumziko lakini Southampton wakafyetuka kwa kasi baada ya mapumziko hayo.
Baada ya magoli mawili ya Austin, Steven Davis alimchenga Jordan Pickford kutoka ukingoni mwa boksi na kuwapa Saints karamu ya magoli hayo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni