Kamati ya Umoja na usalama ya wilaya ya Kibaha leo itafanya mkutano wa hadhara kwenye Kata ya Soga wilayani humo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la mkuu wa mkoa huo Mh. Evarist Ndikilo la kuwaondoa wafugaji waliovamia eneo hilo kiholela.
Afisa usalama wa wilaya ya Kibaha OCD Innocent amethibitisha hilo ambapo ameeleza kuwa tayari wameshakaa kikao cha kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya chini ya Mwenyekiti ambaye ni mkuu wa wilaya Bi Assumpter Mshana ili kuona namna gani watatekeleza agizo hilo.
Aidha OCD Innocent amesema kuwa kwa kuanza leo wanatarajia kufanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Soga ili kujadili na wananchi kabla ya kuanza oparesheni hiyo ya kuwaondoa wafugaji na mifugo yao ambao walivamia bila utaratibu.
Naye kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Blasius Chatanda amesema kuwa amelisikia agizo hilo la mkuu wa mkoa kwenda kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kibaha, lakini wao kama chombo cha usalama cha mkoa wamejipanga kuhakikisha wanatoa ushirkiano wowote utakaohitajika.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mh. Evarist Ndikilo alitoa agizo la kuondolewa kwa wafugaji katika eneo la Kata ya Soga wilayani Kibaha kufuatia mmoja wa wafugaji kuuawa kwa kupigwa risasi baada ya mifugo yake kuingia kwenye shamba la Mohammed Enterprises.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni