Kuelekea mpambano wa Ligi Kuu kati ya Stand United dhidi ya Simba, mashabiki wa timu hizo wamezidi kutambiana kwa kila mmoja kujinasibu kushinda.
Simba inatarajia kujitupa uwanjani kuwakabili Stand United leo saa 10 jioni kusaka pointi tatu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kupanda kieleleni.
Mashabiki wa Simba wakiongozwa na Said Salim wamesema kuwa iwe isiwe lazima mnyama aungurume na pointi tatu ni muhimu.
"Msimu huu ubingwa ni muhimu tuna njaa sana na kombe, kwa hiyo ili tufanikiwe lazima tushinde kila mchezo," amesema Salim.
Naye Shabiki wa Stand United, Lamson Gimy alisema Simba alikuwa na makali kwa kipindi cha nyuma lakini kwa sasa makucha yake yalishakatwa.
"Hana lolote huyo, lazima akalishwe leo tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda" amesema Gimy.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni