Jumatano, 25 Oktoba 2017

TRA yazifungia taasisi na makampuni Tanga

Mamlaka ya mapato nchini (TRA) mkoani Tanga imezifungia taasisi na kampuni za Eckenford za jijini humo baada ya kushindwa kulipa malimbikizo ya kodi mbalimbali hadi mwaka huu .

Akizungumza na waandishi wa habari meneja wa Tra mkoa wa Tanga Masawa Masatu amesema mamlaka ya mapato imeamua kuzifungia kuendesha biashara ikiwa ni hatua ya kwanza ya kuwashinikiza kulipa madeni yao na kwamba endapo wa watashindwa kufanya hivyo hatua inayofuata ni kuuzwa kwa mali zilizozouiwa.

Amesema zoezi la kufungia taasisi na kampunini yanayodaiwa litakua endelevu na kuwataka wafanya biashara wengine kujitokeza ili kuepuka usumbufu.

Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo cha Ekenford Prof John Kiango amesema yatari hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kuhakikisha deni hilo linalipwa katika muda uliopangwa.

Kodi inayodaiwa katika taasisi hizo ni ongezeko la thamani (Vat) kodi inayotokana na malipo ya wafanyakazi (PAE)na kodi ya kuendeleza ufundi stadi (SDL) .



Hakuna maoni: