Mke wa kiungo wa Simba Haruna Niyonzima amemwambia mumewake inabidi aongeze juhudi zaidi ili aendelee kuwafurahisha mashabiki wake.
Mama watoto huyo wa Niyonzima alizungumza na Jacob Mbuya wa Clouds Media Group baada ya mchezo wa Simba dhidi ya Mtibwa Sugar uliomalizika kwa sare ya kufungana 1-1.
“Nampongeza kwa sababu alicheza vizuri kwa namna nilivyoona, lakini naomba aongeze nguvu kwa ajili ya kuwafurahisha wanaompenda.”
Alipoulizwa kuhusu changamoto anazopata kufuatia mumewake kuhama kutoka Yanga kwenda Simba amesema hakuna ugumu anaopitia zaidi ya kubadili marafiki.
“Unajua Niyonzima alicheza kwa muda mrefu Yanga, nilipata marafiki wengi lakini baada ya kuhama sio wote waliokuwa marafiki wakati yupo kule wataendelea kuwepo hadi sasa baada ya kuhama.”
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni