Jumatano, 18 Oktoba 2017

Muungwana Blog yatunukiwa Cheti

Mkuu wa mkoa Paul Makonda kwaniaba ya wananchi wa Dar es salaam amezishukuru taasisi na wadau wote waliochangia kufanikisha kampeni ya zoezi la upimaji afya bure lililofanyika tarehe 6 hadi 10 mwezi Septemba, 2017 katika viwanja vya mnazi mmoja mkoani humo.

Baadhi ya taaisisi za serikali na zisizo za serikali zilizopewa vyeti ni pamoja na Hospitali ya Hindu Mandal, Halmashauri ya Jiji, Taasisi ya Damu salama, taasisi ya madaktari wa kinywa Tanzania Dental Association), TTCL, Kiwanda cha maziwa ya Tanga Fresh n.k.

Vyeti hivyo pia vimetolewa kwa Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii iliyoshiriki kuuhabarisha umma, ni pamoja na TBC 1, mtandao wa MUUNGWANA BLOG sambamba na vyombo vingine vya habari.

Mara baada ya kuwakabidhi vyeti hivyo amewashukuru kwa kusema walifanya kazi yao bila kujali itiadi zao za kidini, Siasa na kikanda, sambamba na kuwaomba waendelee kujitolea kwa moyo mmoja.

 Aidha amesema lengo ilikuwa ni kupima wananchi 10000 lakini walizidi hadi kufikia 14,650 na kuongeza kuwa wasingweza kuwazuia hao walioongezeka.
RC Makonda (Kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani Mwandishi wa Habari wa Mtandao wa Muungwana Blog Habib Shaban.

KWANIABA YA WASOMAJI WETU, TUNATOA PONGEZI ZETU ZA DHATI KWA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MH: PAUL MAKONDA KWA KUTAMBUA MCHANGO WETU KATIKA MAENDELEO YA JIJI LA DAR ES SALAAM. 

Hakuna maoni: