Mbunge wa Mukurwe Anthony Kiai
Mbunge huyo aliyejulikana kwa jina la Anthony Kiai alituma ujumbe wa kimapenzi kwenye group na kuwaomba wabunge wenzake kutoutilia maanani kwani amekosea.
Admin wa group Bwana Bernad Chege, alimuomba mbunge huyo kuomba radhi, na badala yake msaidizi wa Mbunge huyo ndio akaomba radhi kwa kitendo hicho cha bosi wake.
Ujumbe huo ulioandikwa kwa lugha ya Gikuyu ambayo inaongelewa na Wakikuyu nchini Kenya, ilikuwa ikitoa maelezo jinsi kumridhisha mwanamke chumbani, huku baadhi ya wabunge wengine walionekana kumtetea wakisema ngono sio dhambi.
Mbunge Kiai amekuwa mbunge wa jimbo la Mukurweini kufuatia ushindi alioupata kwenye uchaguzi wa Agosti 8, 2017.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni