KOCHA WA KAGERA SUGAR, MECKY MAXIME.
Mechi hiyo namba 44 ya raundi ya sita inatarajiwa kufanyika kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Akizungumza na Nipashe jana, Lwandamina, alisema kuwa wataingia uwanjani kwa tahadhari huku wakijipanga kucheza soka la kiwango cha juu.
"Sitegemei kuwa mchezo wetu utakuwa rahisi, Kagera Sugar watakuwa nyumbani lakini na sisi tunachangamoto ya majeruhi, ila tumejipanga kuhakikisha hatudondoshi pointi," alisema Lwandamina.
Aliongeza kuwa soka ni mchezo wa dakika 90, na kwa upande wake amekiandaa vizuri kikosi chake kwa ajili ya kupambana kwa dakika zote za mchezo huo.
"Siwezi kusema ni mfumo gani nitatumia, lakini tutacheza soka letu tulilolizoea na kuhakikisha tunashinda mechi hii" Lwandamina alisema.
Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, alisema kuwa anaiheshimu Yanga kwa kuwa ni moja ya timu kubwa lakini wamejipanga kutumia vyema uwanja wa nyumbani na kuibuka na ushindi.
"Mpira utakuwa mgumu kwa sababu Yanga si timu ndogo, ila tumejiandaa kufanya vyema kwenye uwanja wetu wa nyumbani na kamwe wasiangalie matokeo ya mechi zetu zilizopita, tusubiri baada ya dakika 90 kujua matokeo," alisema Maxime.
Mechi nyingine za Ligi Kuu Bara zinazotarajiwa kufanyika leo ni kati ya Ndanda FC dhidi ya Majimaji wakati Ruvu Shooting wataikaribisha Singida United na Mwadui FC watavaana na Azam FC huku Lipuli FC ikiwafuata Njombe Mji na Stand United itakuwa jijini Mbeya kuwakabili Tanzania Prisons.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni