Alhamisi, 26 Oktoba 2017

MAFURIKO DAR, Nyumba zafunikwa na maji

Mvua inayoendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam, zimesababisha mafuriko makubwa katika maeneo mbalimbali Jijini humo, ikiwemo eneo la Jangwani ambapo maji hayo yamefunga mawasiliano ya barabara, Hakuna gari inayokwenda wala kurudi mjini.







Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amefika katika eneo hilo nakuwataka wananchi kuondoka katika maeneo hayo kwasasa kwakuwa maji yanaendelea kuongezeka.

Mbunge wa Ilala Musa Zungu amefika na kueleza kuwa mafuriko hayo ni makubwa ingawa mpaka sasa hawajapata takwimu sahihi ya uharibifu unaotokana na mafuriko hayo.



Hakuna maoni: