Jumapili, 29 Oktoba 2017

Kiongozi wa wakurdi nchini Iraq ajiuzulu

Rais wa wakurdi nchini Iraq Massoud Barzani amewacha wadhifa huo wakati eneo hilo linapambana na serikali kufuatia uhuru wake.

Kupitia barua iliyosomwa kwa bunge la Kurdi, Bw. Barzani alisema kuwa hataomba kuongezwa muhula wake ambao unakamilika siku nne zinazokuja.

"Ninaomba bunge kukutana ili kujaza nafasi hiyo," alisema.

Wakurdi walipiga kura mwezi uliopita kuitenga Kurdistan lakini Iraq inasema kuwa kura hiyo ilikuwa kinyume na sheria.




Hakuna maoni: