Jumapili, 1 Oktoba 2017

Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Morogoro yafungia chuo cha uuguzi

Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Morogoro imefungia chuo cha uuguzi cha Tanzanite College of Nursing kinachadaiwa kujiendesha bila kibali huku wanafunzi zaidi ya  300 wakitapeliwa fedha kwa kulipishwa ada zaidi ya shilingi milioni moja na laki tano kwa mwaka, ambapo hata hivyo wanafunzi hao wote wakitokea mikoa ya kanda ya ziwa.

Imeelezwa kuwa chuo hicho kimeanza kutoa huduma hiyo tangu mwaka 2016 ambapo mamlaka husika hazikuweza kutoa kibali kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya kutoa elimu ya uuguzi kwa wanafunzi na badaye kufungiwa lakini hatua hiyo haikutekelezwa.

Baada ya kukamatwa mkuu wa chuo hicho Vedasto Malima na kukuta milango yote imefungwa, mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi, Regina Chonjo ameamuru milango kuvunjwa ili kufanya upekuzi wa nyaraka zilizokiwezesha chuo kiwepo.

Mganga mkuu wilaya ya Morogoro Baraka Jonas ameeleza kwa muda mrefu wamekuwa wakifuatilia uhalali wa kuwepo chuo hicho.


Hakuna maoni: