Madrid, Hispania. Mabingwa wa Kombe la Dunia 2010, Hispania wamefuzu kwa mara 11 mfululizo kwa fainali za mwakani Russia.
Hispania imepata tiketi hiyo baada ya kuifunga Albania kwa mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika jana usiku.
Hispania haijawai kukosa fainali hizo tangu 1974, wakati timu hiyo iliposhindwa kucheza kwa fainali zilizofanyika Ujerumani.
Ni Ujerumani na Brazil ndiyo zimefuzu mara nyingi zaidi kwa fainali hizo kuliko Hispania. Miamba hiyo ya Amerika Kusini imeshiriki fainali zote tangu kuanzishwa kwa Kombe la Dunia 1930.
Kama Argentina itafanikiwa kufuzu kwa fainali hizo basi wenyewe watakuwa wanafuzu kwa mara 12 kucheza Kombe la Dunia.
Kocha wa Hispania, Julen Lopetegui amekuwa na mafanikio tangu alipochukua jukumu hilo, katika mechi tisa za mashindano alizocheza ameshinda nane na kutoka sare moja.
Pia, timu yake imefunga mabao 33 na kuruhusu mabao matatu, rekodi inayowaweka katika mazingira nzuri ya kufanya vizuri katika fainali za mwakani Russia.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni