Mkali wa muziki wa bongo fleva Berry Black ambaye amefanya vizuri na ngoma kibao kali amefunguka na kuweka wazi kuwa kabla ya kifo chake atahakikisha kuwa anarudi tena kwenye muziki na kutoa burudani kwa mashabiki zake kama ilivyokuwa awali.
Berry Black ambaye sasa yupo kimya kimuziki amedai kuwa kwa sasa yeye yupo kwenye mitihani lakini hajaishiwa kimuziki kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakisema kutokana na ukimya wake huo na kudai kuwa kabla ya kifo chake atahakikisha anawapa burudani mashabiki zake.
"Najua wengi wanadhani nimeishiwa kimziki kutokana na kuutafsiri ukimya wangu. Kama binaadamu tupende kuamini kuwa kila mmoja ana mitihani yake. Na anaepanga la kuwa na kutokuwa ni Mungu pekee, hata uwe na watu sabiini wa kukusapoti kama Mungu kakupangia wakati wako, basi ufahamu ndio mpaka uufikie. Kwenye maisha, mfanikio yapo mara mbili, mafanikio yanayokuja pasipo kujiandaa au kupata usumbufu na yale ambayo ulishapoteza kisha ukapambana kila hali, hadi kuyapata" alisema Berry Black
Mkali huyo aliendelea kueleza kuwa
"Haya ya kupambana yana mda mrefu sana na misuko suko mingi. Naamini wapo mashabiki zangu ambao wana subira iliyonipita mimi ila nawaahidi kabla sijaondoka duniani nitawaburudisha na kila walichotamani kukiskia kupitia kipaji changu. Muhimu mnipe sapoti ya kutosha pindi nitaporudi na nawaahidi sitawaangusha" alisisitiza Berry Black
Berry Black siku za karibuni alikuwa chini ya usimamizi wa Mkubwa Fella na alijaribu kutoa kazi kadhaa lakini zilishindwa kufanya vizuri na kumrudisha vyema kwenye ramani ya muziki wa bongo fleva.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni