MADRID, Hispania. Kiungo Andres Iniesta amekuwa mchezaji wa kwanza kusaini mkataba wa maisha wa kuichezea Barcelona, mkataba huo utamfanya acheze klabu hapo wakati wote atakapokuwa fiti.
Klabu huyo ilisema jana kuwa mkataba wa Iniesta umeongezwa kwa maisha yake yote, ataendelea kuwa hapa kwa muda wote wa maisha yake, hakuna kipengele cha kustaafu.
Klabu hiyo haijasema nini yatakuwa majukumu ya Iniesta atakapoacha kucheza.
"Nitakuwa hapa wakati wote ambao mwili na akili yangu itakuwa fiti," alisema Iniesta mwenye miaka 33.
"Ni matumaini yangu hii itakuwa kwa muda mrefu. Mwisho wa msimu tutafanya tathimini ya mambo yote na kuangalia kilichobora kwa kila upande."
Iniesta ameichezea klabu hiyo mechi 639, tangu alipojiunga nayo Oktoba 2002. Akiwa amefunga mabao 55 tangu wakati huo.
Ni Xavi Hernandez aliyecheza mechi nyingi zaidi yake akiwa na mechi 767. Akifutiwa na Lionel Messi ambaye amecheza mechi 594.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni