Alhamisi, 5 Oktoba 2017

Barcelona yagomewa na Atletico Madrid

Klabu ya Atletico Madrid imesisitiza kuwa itawapatia FC Barcelona tiketi kama wanavyofanya kwa timu nyingine za La Liga.

Hii imekuja baada ya wafalme hao wa soka la Hispania Barcelona kuitaka timu hiyo kutowapatia tiketi kwaajili ya mashabiki wao kwa kuhofia kuchomoza vitendo vya vurugu kutokana na maswala ya kudai Jimbo la Catalonia kujitoa Hispania.

Atletico imekiambia chombo cha habari cha Sky Sports kuwa imetoa tiketi za ugenini sawa na timu nyingine la La Liga msimu huu.

 Barca imepatiwa tiketi 250, kwaajili ya mchezo huo utkaofanyika Oktoba 14 katika dimba jipya la Wanda Metropolitano.

Ambapo wamesema hiyo ni sawa na kiasi cha tiketi walichaipatia timu ya Sevilla na Malaga katika michezo ijayo itakayo pigwa katika uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua idadi ya watu 68,000.

Hakuna maoni: