Jumatatu, 25 Septemba 2017

TIBAIJUKA AUNGA MKONO HII LA JPM.

Tokeo la picha la ANNA TIBAIJIKA
Mbunge wa Muleba Kusini(CCM), Anna Tibaijuka amesema ni lazima jamii ikubaliane na agizo la Rais John Magufuli la kuwataka wanafunzi wanaopata mimba kutoendelea na masomo.
Pia, amesema jambo hilo ni lazima liangaliwe katika upana mkubwa ikiwa ni pamoja na kuwaendeleza kimasomo katika taasisi mbalimbali.
Amesena hayo leo Jumatatu katika mahojiano na waandishi kwenye mahafali ya 15 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Barbro Johanson.
Profesa Tibaijuka ambaye pia ni mwenyekiti mwanzilishi wa shule hiyo, amesema kuruhusu wanafunzi wanaopata mimba kuendelea na masomo ni kuongeza tatizo hilo kwa kiasi kikubwa.
"Ni lazima jamii ikubali kuwa sehemu kama shule si mahali ambapo patakuwa na watu wenye mimba," amesema
"Lakini inapotokea, labda kutokana na malezi, ufanyike utaratibu wa kumsaidia aliyeathirika," amesema.
Mkuu wa shule hiyo, Halima Kamote amesema licha ya kuwa na wanafunzi wa kike zaidi ya 600, hakuna aliyepata mimba akiwa shule kutokana na malezi mazuri kwa kushirikiana na wazazi.
Amesema jumla ya wanafunzi  116 watahitimu kidato cha nne na kwamba wamejifua kitaaluma kukabiliana na mtihani wa Taifa.


Hakuna maoni: