Klabu ya Simba haijatoa taarifa yeyote kuhusiana na mabadiliko yanayoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wasioitakia mema klabu yetu.
‘Nimeshaeleza toka awali kuwa, hakuna mechi tano wala huo mpango wa kumwondoa kocha Omog au benchi zima la ufundi, klabu ya Simba haina mpango huo.
'Tunaomba mashabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Simba kuweka Imani yao kwa Uongozi, kikosi cha Simba na benchi la ufundi kuwa tunajua nini mashabiki wetu wanachotaka na ndicho tunachopambana kuhakikisha tunafikia malengo' alisema Haji Manara alipoongea na Simba News kuhusiana na ujumbe unaosambazwa wa kuvunjwa kwa benchi la ufundi la Simba.
Klabu ya Simba itaendelea kuhakikisha inatoa taarifa sahihi na kwa wakati kupitia njia zake za mawasiliano chini ya Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Haji Manara na sio kwingineko.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni