Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo anawatangazia Wafanyabiashara Wote wa Viwanda Vidogovidogo Dar es Salaam kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupatiwe Mkopo wenye Riba Nafuu ili kukuza Biashara zao kufikia kiwango cha Kati kisha kuwa na Viwanda Vikubwa.
Hatua hiyo ni baada ya RC Makonda kufanya mazungumzo jana na Mfuko wa hifadhi ya Jamii NSSF kuhusu kuwekeza Wafanyabiashara wadogo Mkoa wa Dar es salaam ambao baada ya mazungumzo hayo NSSF imemkubalia kutoa fedha za kutosha kwaajili ya kuwakopesha wenye Viwanda Vidogovidogo
Kwa mantiki hiyo Makonda amewataka Wafanyabiashara hao kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuonana na Afisa Biashara wakiwa na Mchanganuo wa Biashara zao kisha kueleza kiwango cha Fedha wanazotaka kukuza Biashara zao na kuongeza uzalishaji.
Mheshimiwa Makonda amesema lengo la Mpango huo ni kuwawezesha Wafanyabiashara kuwa na Mitaji itakayowafanya kukuza Viwanda vyao ili kufikia malengo na azma ya Rais DR.John Magufuli ya kuwa na Tanzania ya Viwanda.
Katika juhudi za kuwakwamua Wafanyabiashara wazawa Makonda ameeleza mpango wa kuanzisha Soko la kuonyesha na kuuza bidhaa zinazozalishwa na wazawa kila Mwezi mara Moja kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Aidha Makonda amezielekeza Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha 10% ya fedha zinazotengwa kwaajili ya kuwakopesha Kinamama, Vijana na Walemavu zinatolewa kwa Wafanyabiashara wenye Viwanda Vidogovidogo ili kuwaongezea nguvu.
Katika hatua nyingine RC Makonda amewataka Wamachinga kutoa kipaombele kwa kuuza Bidhaa zinazozalishwa na Wafanyabiashara wazaw ilikukuza uchumi wa Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni