Wapinzani wa Yanga katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya soka ya Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar wamebainika usiku huu baada ya klabu hiyo kumaliza ya pili hivyo kukutana na URA.
Yanga imekubali sare ya 1-1 kutoka kwa Singida United hivyo kufikisha alama 13, ambazo zinaifanya kumaliza ikiwa na nafasi ya pili nyuma ya Singida yenye alama 13 zikitofautiana idadi ya mabao.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuanguka mikononi mwa URA ya Uganda ambayo jioni ya leo imeitupa nje Simba SC na kutinga hatua ya nusu fainali ikiwa kinara wa kundi B.
Singida United ambayo imeshinda mechi nne kati ya tano za kundi A itakutana na Azam FC ambayo imeshika nafasi ya pili katika kundi B nyuma ya URA.
Mechi za nusu fainali zitapigwa Januari 10 ambapo moja itaanza majira ya saa 10:00 jioni, kabla ya mechi ya pili kupigwa saa 2:00 Usiku. Mechi ya fainali itapigwa Januari 13 siku ya Jumamosi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni