Jumanne, 9 Januari 2018
Singida United yatoa siri
Baada ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar klabu ya Singida United imefichua siri kuwa haikuwa rahisi kwa wao kushiriki michuano hiyo pamoja na kuonesha nia hiyo mapema.
Klabu hiyo ambayo imepanda ligi kuu msimu huu, kupitia kwa Mkurugenzi wake Festo Sanga wamesema baada ya kuwa na nia ya kushiriki michuano hiyo ilibidi waanze kuiomba kamati ya maandalizi ya michuano hiyo iwape nafasi kitu ambacho haikuwa rahisi ilibidi kuwahakikishia kuwa watafanya vizuri.
''Kushiriki michuano ya Mapinduzi kimsingi ni jitihada binafsi za viongozi wa klabu na viongozi wa mapinduzi Cup, tulikuwa tunawasiliana nao tangu mapema kabla hata ya michuano kuanza na wao wakakubaliana wakatukaribisha na tuliwaahidi kuwa tutajitahidi kuonysha uwezo wetu'', amesema Sanga.
Singida United iliyopangwa kundi A na timu za Yanga, Zimamoto, JKU na Taifa Jang'ombe imeshinda mechi nne za kundi hilo na kutoka sare ya 1-1 na Yanga hivyo kuwa kinara wa kundi hilo.
Singida United itashuka dimbani kesho kukipiga na Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali ya Mapinduzi. Kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara Singida United inashika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam FC.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni