Rage
May 17 2012 taarifa za kifo cha mchezaji waSimba raia wa Rwanda Patrick Mutesa Mafisango zilianza kusambaa baada ya awali kuripotiwa kuwa amepata ajali na kukimbizwa hospitali lakini madaktari wakathibitisha kuwa amefariki.
Uongozi wa Simba kwa heshima wakatangaza kuwa jezi namba 30 iliyokuwa inatumiwa naMafisango wameistafisha kwa heshima haitavaliwa tena na mchezaji yoyote katika club ya Simba SC, hivyo baada ya jana jezi namba 30 kuvaliwa na golikipa wa SimbaMseja.
Golikipa Mseja aliyevaa jezi namba 20 jana
Rais wa zamani wa Simba SC Ismail Aden Rage ameulizwa kuhusu jezi hiyo kupewa mchezaji mwingine amesema haya
“sasa hii ungewatafuta viongozi wa sasa ukawauliza mimi pia nimeshituka nilipoona maana sijui hao watu walikuwa wapi wakati ule lakini sisi hatukufuta uamuzi huo ndio maana umeona jezi hiyo ikitumika jana”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni