Mwandishi na Mpiga picha wa Muungwana Blog/TV, Abubakary Mkoba ameaga rasmi Timu ya makapela baada ya kufunga Ndoa na Mchumba wake wa muda mrefu, Zakia Hamis Wadi. Harusi hiyo ilifanyika maeneo ya Magomeni mkoani Mtwara Januari 7, Mwaka huu.
Uongozi na Wafanyakazi wa Muungwana Blog wanamtakia Ndugu Mkoba na Mkewe Zakia maisha marefu yenye usikivu, uvumilivu, furaha na upendo ndani ya Ndoa yao na kuwakumbusha kumtanguliza Mwenyezi Mungu katika kila jambo. Hongera Mkoba hongera Zakia.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni