Jumanne, 9 Januari 2018

MUM CUP:GARAGE FC YATINGA FAINALI

 



Na Shaban Khamis,Morogoro
Michuano ya MUM CUP ndani ya Chuo kikuu Cha waislamu Morogoro imeendelea leo kwa mchezo wa nusu fainali kati ya Garage Fc dhidi ya Diplomo in laboratory.

Mechi hiyo ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa imemalizika kwa Garage FC kuibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja(2-1).

Magoli yote ya Garage yamefungwa na mshambuliaji matata,Alik Hemed maarufu kama Kante huku goli la kufutia machozi la Diploma likifungwa na Omary.

Nusu fainali ya pili itapigwa hapo kesho ,Eleven Boys watavaana na Mwaka wa pili majira ya saa kumi jioni.

Michuano hiyo itafikia tamati siku ya ijumaa kwa mchezo wa fainali kati ya Garage Fc na mshindi atakaepatikana kwenye mchezo wa Kesho


Hakuna maoni: