Jumanne, 9 Januari 2018

Mama Mobetto atoa ya moyoni sakata la kuporwa Bwana na Bi Sandra

Mama Mobeto.

 KWA siku kadhaa kumekuwa na ubuyu mzito kuwa, mwanaume anayedaiwa kumuona mama wa msanii wa Bongo Fleva, Sanura Kassim almaarufu Bi Sandra anayetambuliwa kwa jina la Salum Shamte aliporwa kutoka kwa mama mzazi wa mwanamitindo wa kimataifa Bongo, Hamisa Mobeto, Shufaa Lutingunga, Ijumaa Wikienda limeichimba.

Kufuatia tuhuma hizo nzito, Ijumaa Wikienda liliingia mzigoni kusaka ukweli wa ishu hiyo ambapo lilifanikiwa kumweka ‘mtukati’ mama Mobeto ambaye aliyafungukia madai hayo.

Mama Mobeto aliliambia gazeti hili kuwa, siku hizi ameamua kukaa kimya kwa sababu akiwa anafuatilia kila

 kitu kinachoandikwa kwenye mitandao ya kijamii, anaweza kupoteza maisha huku siku zake zikiwa bado hazijafika.

Mama huyo alifunguka kuwa, mwanaume huyo aliyemuoa Bi Sandra anamfahamu kama rafiki, lakini hajawahi kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Alisema kuwa, jambo hilo halikuwahi kutokea hata mara moja hivyo anashangaa watu wanavyopandikiza maneno.

“Huyo kaka (Shamte) ninamjua kama rafiki yangu tu na hatukuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi hata mara moja.

“Ninashangaa mno kuona au kusikia watu wanakomalia kuwa mimi nilikuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

“Lakini siku zote mtu akiamua kusema, ninamwacha aseme au afanye awezavyo,” alisema mama Mobeto.

Kwa upande wake Bi Sandra hakupatikana hewani ili kusikia upande wake hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.
BI Sandra na Mumewe.


Hakuna maoni: