Jumanne, 9 Januari 2018

Kesi ya wanawake waliovishana pete yaahirishwa

Shauri linalowakabili watu wanne kwa kufanya vitendo vinavyoashiria mapenzi ya jinsia moja na makosa ya kimtandao limeharishwa hadi Februari 5, mwaka huu litakapotajwa tena.

Akiahirisha shauri hili jana, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza Veronica Mugendi, alisema hakimu mwenye dhama ya kusikiliza shauri hilo Hakimu mkazi Mwandamizi mfawidhi Wilbert Chuma yupo likizo.

Washtakiwa katika kesi hiyo namba 548/2017 ni Milembe Suleiman na Janeth Shonza ambao  wanadaiwa kuvishana pete ya uchumba licha ya kwamba wote ni wanawake.

Wengine ni Aneth Mkuki anayeshtakiwa kwa kosa la kufanikisha sherehe hizo na Richard Fabian anayeshatakiwa kwa kosa la kusambaza video za sherehe hiyo.

Washtakiwa hao walipata dhamana desemba 15 mwaka jana baada ya kukamilisha dhamana.




Hakuna maoni: