Jumatano, 10 Januari 2018

Hii ndio sababu polisi kukamata wajawazito


Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara Sebastian Waryuba , ametolea ufafanuzi suala lililoleta sintofahamu kwa jamii, la kuwakamata mabinti wanafunzi waliopata ujauzito na kuwapeleka polisi.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Mheshimiwa Waryuba amesema amefikia uamuzi wa kufanya hivyo ili kuweza kuisaidia serikali kubaini watu waliosababisha kukatisha masomo kwa mabinti hao, ambao mara nyingi wamekuwa wakihofia kuwataja.

Mheshimiwa Waryuba amesema kuwa mabinti hao pamoja na wazazi wao wametoa ushirikiano wa kutosha kwa serikali kwa kuwataja, huku wakionyesha kujutia baada ya kufikishwa polisi, lakini wote waliachwa huru baada ya kukamilisha mahojiano.

Hakuna maoni: