Jumatano, 10 Januari 2018

Dar yashinda tuzo ya usafiri bora

Jiji la dar es Salaam limepata tuzo ya mwaka ya huduma bora ya usafiri endelevu kupitia mradi wake wa mabasi yaendayo haraka DART kwa kuleta mabadiliko ya haraka katika kutatua changamoto ya msongamano wa magari uliokuwa ukilikabili jiji hilo.

Dar es Salaam linakuwa la kwanza kupata tuzo hiyo  ya kimataifa kwa nchi za Afrika  kwa  kipindi cha miaka 13,inayotolewa katika hafla iliyofanyika majira ya asubuhi mjini Washington DC nchini Marekani.

Hakuna maoni: