Jumatatu, 8 Januari 2018

Bolt haishiwi vituko, kujfanya majaribio Dortmund

Nyota wa zamani wa riadha duniani Usain Bolt, amesema amepona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu, na sasa yupo mbioni kufanya majaribio kwenye klabu ya Borussia Dortmund.

Bolt mwenye umri wa miaka 31, amesema mwezi Machi atafanya majaribio ili kujua nini anahitaji kuongeza ili aingie rasmi kwenye soka la ushindani, ambayo ilikuwa ndoto yake ya muda mrefu, huku akisema lengo lake ni kuichezea klabu anayoishabikia ya Manchester United.

"Mwezi Machi nitafanya majaribio kwenye klabu ya Dortmund, hatua ambayo itaamua nini cha kufanya ili niwe mchezaji kamili, na wakisema mimi ni mzuri basi nitaanzia hapo kuhakikisha ndoto yangu ya kuchezea Manchester United inatimia'', amesema Bolt.

Bolt ambaye ni raia wa Jamaica, anahesabiwa kama mwanariadha bora zaidi kuwahi kutokea baada ya kushinda medali za dhabau kwenye michuano nane tofauti ya Olimpiki.

Hakuna maoni: