Jumatano, 10 Januari 2018

Ali Kiba ampa nguvu Hussein Machozi


Msanii Hussein Machozi ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Sweet Melody' amefunguka na kusema kuwa kitendo ambacho amefanya msanii Alikiba kumpa 'support' katika kazi yake hiyo kimempa nguvu zaidi na kuona na yeye ni mtu muhimu.

Hussein Machozi amesema hayo wakati akiongea na mwandishi wa WWW.EATV.TV na kusema anaamini Alikiba amesikiliza na kuiona kazi yake mpya na kuikubali ndiyo maana ameamua kumpa support.

Msikilize hapo chini akifunguka mengi zaidi juu ya Alikiba na kitendo alichofanya Alikiba kwake kutokana na kazi yake hiyo

Hakuna maoni: