Timu ya Chuo kikuu cha Zanzibar imefanikiwa kuingia hatua ya fainali ya michuano ya vyuo TUSA inayofanyika Dodoma baada ya kuwaondoa chuo kikuu Iringa kwa mikwaju ya Penaiti 4-3 huku kila timu ikipiga mikwaju saba.
Wachezaji wa Timu ya Zanziba
Kufuatia ushindi huo,Kocha mkuu wa Zanzibar,Juma Yusuph Khamis amesema pongezi ziwafikie viongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuweza kumsafirisha golikipa wao Ahmed Ally Suleiman (kutoka Zanzibar hadi Dodoma) aliyekuwa akishiriki mashindano ya CECAFA nchini Kenya.
Ahmed Suleiman(Salula) amesema amefarijika kwa mapokezi aliyoyapata kutoka kwa watanzania baada ya kutua uwanja wa ndege wa Dodoma kwa ajiri ya kuitumikia timu yake ya Chuo cha Zanzibar.
Timu nyingine iliyofuzu kuingia Fainali ni Chuo kikuu cha Mtakatifu John (St.John) baada ya kuwaondoa Chuo kikuu Mkwawa .
Mchezo wa Fainali kati ya Zanzibar na St.John utafanyika hapo kesho
Kwa upande mwingine mapema leo kulikuwa na michuano ya Riadha ambapo Rashid Omary Muna kutoka Chuo kikuu Iringa aliibuka mshindi kwa upande wa wanaume mbioo za mita 5000 akitumia dakika 15 na sekunde 15. Muna amewahi kushiriki michuano mbalimbali hapa nchini ikiwemi Kilimanjaro Marathon 2017 na KIA marathon 2017.
Rashid Omary Muna,Mshindi wa riadha upande wa wanaume
Riadha upande wa wanawake mshindi ni Salome Imani Luvanda wa chuo kikuu Huria Singida aliyeshinda mbio za mita 100 na 200.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni