Waziri wa Kazi, Mawasiliano na uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, amewatakia Watanzania wote duniani heri ya sikukuu ya Chrismas na mwaka mpya, na kutoa agizo kwa wale wanaotumia vyombo vya moto kuwa makini barabarani.
Profesa Mbarawa ametoa agizo hilo kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa twitter, na kusema kwamba kwa kipindi hiki cha sikukuu kimekuwa na changamoto kubwa za usafiri, ikiwemo kutozwa nauli ya juu, na kuwataka kutoa taarifa mara moja kwa vyombo husika.
"Napenda kuwatakia Watanzania wote kila la kheri katika msimu wa sherehe za Xmas & mwaka mpya 2018,wito wangu kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri kuzingatia Sheria na Kanuni za barabarani, aidha, kipindi hiki cha msimu wa sikukuu kumekuwa na changamoto ya usafiri hivyo kwa abiria endapo utatozwa nauli za juu ya viwango vilivyowekwa usisitize kuripoti usijisikie muhali kuripoti kwenye vyombo husika kwa wakati", ameandika Profesa Mbarawa.
Hivi karibuni kumekuwa na tatizo la wamiliki wa vyombo vya usafiri kuongeza bei ya nauli kutokana na wingi wa watu wanaofanya safari zao kuelekea mikoani kusherehekea sikukuu za mwisho mwaka, na kufanya kuwa na ugumu wa usafiri.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni