Jumanne, 19 Desemba 2017

WATU WAMZUSHIA KIFO HAJI MANARA,MWENYE AIBUKA KUKANUSHA



Mkuu wa idara ya habari ya Simba, Hajima Manara ameibuka kukanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao kuwa yeye amefariki.

Manara amekanusha taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa huku akitoa pole kwa wote walioguswa na uzushi huo.


"Taarifa zinazoenezwa mitandaoni juu ya uhai wangu c kweli.nipo hai na mzima wa afya kwa uwezo wa Mungu..poleni nyote mliokuwa msibani kwa kupewa taarifa isiyo sahihi...poleni pia familia yangu.hususan mama na dada zangu.🙏🙏" Ameandika Haji manara kwenye Ukurasa wake wa Instagram

Taarifa hiyo  ambayo chanzo chake ni Mtandao wa Facebook iliandikwa na mtumiaji aliyefahamika kwa jina la "Mudrick Likoswe Mtwara" na kuituma  kwenye Group la "Michezo Extra" kama inavoonekana hapa chini



Hakuna maoni: