Serikali imeshauriwa kuboresha huduma zinazotolewa na Bima ya AFya ya Jamii NHIF ili ziendane na huduma za matibabu zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIFí ili kumuwezesha Mwanachama wa bima ya AFya ya Jamii kupata matibabu sawa na Mwanachama wa NHIF
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Oran Njeza anatoa ushauri huu akiwa katika Hospitali Teule ya Mbalizi, ambako ametoa msaada mbalimbali kwa wagonjwa ikiwa ni kusherehekea pamoja nao sikukuu ya Noel , akiwa ameongoza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Jackobo Mwakasole na Uongozi Chama cha Mapinduzi Wilaya na Makanda wa chama hicho.
Muunguzi Mfawidhi wa Hospital Teule ya Mbalizi Helmath Sanga anasema katika mkesha wa sikukuu ya Noel watoto kumu wamezaliwa.
Awali Mbunge huyo akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Uongozi wa Wilaya na Makanda wa CCM wa mefanya usafi katika Hospital teule ya Mbalizi na Badaye kutembelea wagonjwa na kugawa zawadi ya sikukuu ya noel ambapo baadhi ya zawadi ni sabuni, mafuta ya kupakaa, soda na juice lakini pia akaupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanazofanya.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni