Jumanne, 26 Desemba 2017

MPIGA PICHA WA AZAM TV AFARIKI DUNIA



Mpigapicha maarufu wa runinga ya Azam TV, Idd Salum Mambo amefariki dunia baada ya kuugua muda mfupi.

Mambo amefariki dunia akiwa kikazi  jijini Mwanza ambako aliwasili jana na mauti kumkuta usiku wa kuamkia leo.

Mmoja wa viongozi wakuu wa Azam TV, Baruan Muhuza amesema marehemu anatarajia kuzikwa leo katika makaburi ya Kawe jijini Dar es Salaam.


Hakuna maoni: