Jumamosi, 16 Desemba 2017

MCHEZO YA KIRAFIKI KATI YA YANGA NA POLISI YASOGEZWA MBELE


Mechi ya kirafiki iliyopangwa kuchezwa kesho Jumamosi kati ya Yanga na Polisi Tanzania itachezwa keshokutwa Jumapili.

Awali, mechi hiyo ilipangwa ichezwe kesho Jumamosi maalumu kwa Yanga kuangalia nyota wake baada ya kufanya mazoezi.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata mechi hiyo ambayo imepangwa kuchezwa uwanja wa Taifa imeahirishwa kutokana na nyasi kufyekwa bila ya viwango ambazo ni fupi zaidi.

Meneja Mkuu wa Yanga, Hafidh Saleh alithibitisha hilo kwa kusema kuwa "Mechi yetu tuliyopanga tucheze kesho Jumamosi itachezwa Jumapili na siyo Jumamosi kama tulivyopanga baada ya kutokea matatizo.


Hakuna maoni: