Jumamosi, 23 Desemba 2017

Dk Mahenge awaagiza watendaji kutenga muda kusikiliza kero za Wananchi


Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewaagiza watendaji kutenga muda kusikiliza kero za wananchi.

Dk Mahenge ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Desemba 23,2017 alipofungua kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC).

Amesema katika maeneo ambayo ametembelea amegundua baadhi ya watumishi hawatimizi wajibu, hivyo kusababisha kero kwa wananchi.

Dk Mahenge amesema changamoto anayoipata anapowatembelea wananchi ni vilio vya kukosa msaada kutoka kwa watumishi.

"Maeneo mengine utakuta mtu anahitaji ushauri tu lakini hapati mtendaji wa kumshauri, nendeni mkasikilize kero za watu," amesema Dk Mahenge.

Pia, amewaagiza watumishi wa umma kuhakikisha maeneo yao yanakuwa na  utulivu na amani.

Hakuna maoni: