Jenerali wa Zimbabwe, aliyeongoza mapinduzi yaliyopelekea Robert Mugabe kuondoshwa madarakani, ameteuliwa kuwa naibu kiongozi wa chama tawala cha ZANU-PF.
Uteuzi huo ulifanywa na rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa.
Constantino Chiwenga, alistaafu hivi karibuni kama mkuu wa jeshi, na kuzusha tetesi, kwamba atapewa wadhifa wa kisiasa.
Uteuzi huo, unaonekana kama hatua ya kuelekea kutajwa kuwa makamo rais.
Naibu mwengine wa chama ni Kembo Mohadi.
Alikuwa waziri wa usalama wa taifa, katika serikali ya bwana Mugabe, ambaye aliongoza nchi kwa karibu miongo mine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni