Jumatatu, 27 Novemba 2017

Wananchi Dar kupewa kinga tiba bure


Kikao cha uragibisho wa kunywa dawa za matende, mabusha na minyoo ya tumbo kimefanyika leo jijini Dar es salaam kwa kutoa mafunzo na maada kwa watendaji wa serikali ili kujenga uwezo wa ndani kwa kujipanga kuepuka kusubiri wafadhili.

Kikao hichi kilichofunguliwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda amewapongeza madaktari kwa kazi nzuri wanayofanya kwani zoezi limefanyika hili pia lilifanyika mwaka jana chini ya wizara ya afya kwa kuona umuhimu wa magonjwa hasa yasiopewa kipau mbele na kuleta shida kwa jamii  kwa kukatisha ndoto.

"maeneo ya pwani kwa magonjwa haya sio kitu cha ajabu sana hivyo kama mkoa lazima tujipange na kuweka mikakati kwa kujenga uwezo wa ndani kwa kuwahudumia wagonjwa wetu", alisema Mh, Makonda.

Mh, Makonda alitoa rai kwa watu wanaopotosha jamii kwa kusema dawa hizo zinapunguza nguvu za kiume na kwamba sio mda sahihi wa kusema hayo kwani serikali ina lengo zuri kwa wananchi wake na wanahitaji kuona wako na amani na furaha mda wote.

Aidha kwa upande wake dokta GRACE MAGEMBE amesema kuwa katika kutekeleza azima hii ya kugawa dawa za kinga tiba bure, wamepitia hatua mbalimbali kwa kutoa mafunzo, kugawa dawa kwa wilaya zote pia  wanahamasisha wadau wote ambapo kesho utafanyika uzinduzi rasmi eneo la Kigambo, jijini Dar es salaam.

Kutokana na takwimu zinavyoonyesha lengo la wizara ni kuhamasisha jamii  kutumia dawa hizi kama mkoa una wagonjwa wengi ambapo  takribani watu 2222 wanaugua matende na 4162 wakiugua mabusha.

Pia kutokana na takwimu hizi watu wanashindwa kufanya kazi zao vizuri, kwa kutambua hilo serikali ina malengo ya kuhamasisha jamii kutumia kinga tiba ili kuondoa maradhi haya.

Kwa kuzingatia lengo la kuwafikia wananchi wote kutakuwa na vituo katika maeneo mbalimbaliu ya wazi ikiwezo vituo vya mabasi, sokoni, hospitalini, kambi za jeshi na ofisi za serikali za mitaa, hivyo wananchi wote kuanzia miaka mitano na kuendelea wajitokeze kupata kinga tiba ya mabusha, matende na minyoo ya tumbo.



Hakuna maoni: