Jumatatu, 20 Novemba 2017

WANAJESHI 44 BADO HAWAJULIKANI WALIPO ARGETINA



Wanajeshiwa Argentina wakifanya yao.

NYAMBIZI ya Argentina ambayo ilitoweka na wanajeshi 44 bado inaendelea kutafutwa na Wizara ya Ulinzi ya nchini humo, ili kubaini ilipo nyambizi hiyo. Argentina imekuwa ikiitafuta nyambizi yake Kusini mwa Bahari ya Atlantic huku ndege ya utafiti ya Shirika la Nasa ikisaidia shughuli hiyo.

Nyambizi hiyo inayotumia mafuta ya dizeli ilitoweka umbali wa kilomita 430 kutoka pwani.
Uingereza na nchi za eneo hilo zimejitolea pia kusaidia kazi hiyo. “Hatujafanikiwa kuipata, wala hatuna mawasiliano na nyambizi hiyo,” alisema Msemaji wa Jeshi la Wanamaji, Enrique Balbi wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Nyambizi hiyo ilikuwa ikirejea kutoka safari ya kawaida kutoka Kusini mwa Amerika ya Kusini ikielekea kituo chake cha Mar del Plata kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo. Nyambizi hiyo ilizinduliwa mwaka 1983 ndiyo mpya zaidi kati ya nyambizi tatu za Argentina
Buenos Aires, Argentina


Hakuna maoni: