Taifa Stars inakwenda Benin bila ya nahodha wake, Mbwana Ally Samatta ambaye ameumia goti na atatakiwa kukaa nje kwa wiki sita akipata matibabu.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema kuwa wachezaji wote wameshaingia kambini kasoro nahodha, Mbwana Samatta ambaye ni majeruhi pamoja na Abdi Banda.
“Kikosi cha timu yetu ya taifa kinatarajia kuondoka hapa keshokutwa (kesho), Novemba 9, alfajiri kwenda Benin kwa ajili ya mechi yao ya kimataifa ya kirafiki na kitakapofika rasmi kesho yake kitaendelea na programu yake mazoezi huko Benin,” alisema Lucas.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni