Ligi kuu ya Vodacom Tanzani bara imeendelea tena leo wa mchezo mmojakati ya Simba na Lipuli Fc,mchezo uliofanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.
Mchezo huo umemalizika kwa timu zote kuondoka na point moja kila moja baada ya kutoka sare ya kufungana goli moja kwa moja.
Simba ilikuwa ya kwanza kupata goli katika dakika ya 15,goli liliofungwa na Mwinyi kazi moto, dakika mbili baadae Lipuli walisawazisha kupitia mchezaji wao Asante Kwazi.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, msemaji wa timu ya Simba ,Haji manara amesema kwamba ipo haja sasa ya TFF kutoa adhabu kali ikiwemo kufungiwa kabisa kwani wao ndio wanaovuruga michezo.
Manara amesema licha ya wachezaji wa Simba kukosa nafasi za wazi lakini mwamuzi amekuwa kikwakozo kwenye mchezo huo.
Zifuatazo ni picha mbalimbali za mchezo huo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni