Jumatatu, 13 Novemba 2017

Sheikh Kishki atoa taarifa muhimu kwa waislamu

Mhadhiri Mkuu wa Mawaidha ya Kiislam Duniani Sheikh Nurdin Kishki ametoa taarifa kwa umma kwamba kwa sasa anapatikana katika mitandao ya kijamii mara baada ya waumini wengi wa dini hiyo kumuomba ajiunge na mitandao hiyo ili kuweza kuwapatia elimu ya dini hasa wale waishio mbali na yeye.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zake za shule ya Al-hikma jijini Dar es salaam , Kishki amesema kitu ambapo pia kilichomsukuma kujiunga na mitandao ili iwe rahisi kwa waumini kumfikia kwa urahisi sambamba na kupata mawaidha yake.

Kishki amesema kwa sasa anapatikana katika mitandao yote ya kijamii ikiwamo facebook,twitter,Instagram sambamba na kuanzisha Televisheni ya mtandaoni (Youtube channel) iitwayo kishki online tv ,ambapo amesema televisheni haitolenga jamii ya kiislamu pekee  bali itakuwa ni jamii yote kwa ujumla kutokana wadau wengi wanaomuunga mkono ni waislamu na wasio kuwa waislam.

  Amesema jamii itarajie kupata mambo mbalimbali ikiwamo mawaidha ambayo itakuwa na uwezo wa kufuatilia kwa mtu yeyote hata asie kuwa muislam.

Amefafanua kuwa kutakuwemo na mihadhara mbalimbali zikiwamo khutba za ijumaa, usomaji wa qurani tukufu ambapo usomaji huo utasomwa kwa sauti mbalimbali.

Aidha amesema hapo awali watu wengi walikuwa wakilitumia jina lake katika mitandao ya kijamii kinyume na matakwa yake hali ambayo pia imemsukuma kujiunga na mitandao hiyo.

Hakuna maoni: